Ticha SmartTicha Smart
For Teachers

Mwongozo kwa Walimu: Jinsi ya Kutumia Ticha Smart

George Chikao

George Chikao

Platform Updates

23 Aug 20264 min read
Mwongozo kwa Walimu: Jinsi ya Kutumia Ticha Smart

1. Jisajili na Ujaze Maelezo Yako ya Msingi

Nenda kwenye "Become a Teacher" na jaza fomu ya usajili, jina lako kamili, barua pepe, namba ya simu, na taarifa za msingi za taaluma yako. Baada ya kuthibitisha namba yako ya simu kwa msimbo (SMS), akaunti yako itaundwa na maombi yako yataingia kwenye foleni ya ukaguzi wa Admin.

Kidokezo: Hakikisha barua pepe na namba ya simu ulizoweka ni sahihi hapo ndipo taarifa zote muhimu (ikiwemo hongera za kukubaliwa na kupata tick) zitakapokufikia.

2. Chagua Aina Sahihi ya Ufundishaji

Wakati wa usajili, utaulizwa uchague masomo unayofundisha:

  • Elimu ya Kawaida (Academic): Kama unafundisha masomo ya shule Primary, O-Level, au A-Level chagua curriculum na masomo husika (mfano Hisabati, Kiingereza, Physics).

  • Vocational & Digital Skills: Kama una ujuzi maalum (siyo wa shule) kama Digital Marketing, Video Editing, Graphic Design, Ujasiriamali, na kadhalika, chagua kundi hili. Hapa hutahitajika kuweka historia ya shule/chuo badala yake utaweka vyeti vinavyothibitisha ujuzi wako maalum (mfano cheti cha kozi ya Digital Marketing).

Chagua kwa uangalifu hii ndiyo itakayoamua wanafunzi gani watakuona kwenye utafutaji wao.

3. Weka Bei Yako kwa Umakini

Bei yako ("Hourly Rate") ndiyo itakayoonekana kwa wazazi na wanafunzi. Weka bei ya kweli na inayoendana na soko — bei ndogo mno inaweza kuonekana ya kutilia shaka, na bei kubwa mno inaweza kukukosesha wateja. Unaweza kuibadilisha wakati wowote kwenye ukurasa wako wa Profile, kwenye sehemu ya "Hourly Rate" — bonyeza "Edit", weka namba mpya, kisha "Save".

Muhimu: Hakikisha unaandika namba sahihi kabla ya kubonyeza Save angalia mara mbili kabla ya ku-confirm ili kuepuka makosa ya kuandika (mfano sifuri za ziada).

4. Kamilisha Uthibitisho (Verification) Ili Upate Tick

Hii ndiyo hatua muhimu zaidi kwenye safari yako. Baada ya maombi yako kukubaliwa, nenda kwenye "Verification" kwenye dashboard yako na ukamilishe:

  1. Taarifa za utambulisho: jina kamili, namba ya NIDA, na picha za NIDA (mbele na nyuma) pamoja na picha yako ya passport.

  2. Anwani: mkoa, wilaya, kata, na mtaa unapoishi.

  3. Vyeti (Certificates): pakia angalau cheti kimoja kinachothibitisha taaluma/ujuzi wako.

  4. Wadhamini (Guarantors): weka wadhamini wawili watakaothibitisha uaminifu wako.

  5. (Kwa walimu wa masomo ya shule tu) Curriculum chagua mtaala unaoufundisha.

Baada ya Admin kukagua na kukubali, utapata "Verified" tick kwenye profile yako hii inakufanya uonekane wa kuaminika zaidi kwa wazazi na wanafunzi, na profile zilizo na tick huonekana juu zaidi kwenye matokeo ya utafutaji (Ranking Higher).

5. Weka Ratiba Yako ya Upatikanaji

Kwenye sehemu ya "Availability", weka siku na muda unaopatikana kufundisha. Wazazi na wanafunzi wataona muda huu wanapotaka ku-book somo nawe — hivyo hakikisha unaiweka sahihi na kuisasisha mara kwa mara.

6. Pokea na Jibu Maombi ya Masomo (Bookings)

Mzazi au mwanafunzi akiomba somo, utapokea taarifa. Nenda "Schedule" kuona ombi na uamue kukubali au kukataa. Jibu haraka iwezekanavyo — familia inasubiri jibu lako, na kuchelewa kunaweza kuathiri uzoefu wao na hata rating yako.

Baada ya kukubali, familia italipa kupitia mfumo malipo hayo hayatakwenda kwako moja kwa moja mpaka mfumo uyathibitishe.

7. Fundisha kwa Wakati na kwa Weledi

  • Kwa masomo ya Home, hakikisha unafika kwa wakati mahali palipopangwa.

  • Kwa masomo ya Online, tumia sehemu ya "Online Teaching" kuanzisha video call na mwanafunzi wako moja kwa moja kwenye jukwaa.

  • Kama unahitaji kufundisha nyumbani na kushirikisha mahali ulipo, unaweza kutumia "Live Tracking" ili mzazi/mwanafunzi aone unakoelekea.

Kufundisha kwa wakati na kwa umakini kunaongeza rating yako na kukuletea wateja zaidi kupitia maoni mazuri (reviews).

8. Fuatilia Maendeleo ya Wanafunzi

Tumia sehemu za "Homework", "Assessments", na "Progress" kuweka kazi za nyumbani, kupima maendeleo, na kuandika maoni ya ufuatiliaji (progress notes) kwa kila mwanafunzi. Hii inaongeza thamani ya huduma yako na kuwapa wazazi imani zaidi kwako.

9. Uza Vitabu na Nyenzo Zako (Resources)

Una vitabu vya PDF, notes, au nyenzo nyingine za kujifunzia? Nenda "Resources" na uweke (upload) nyenzo hizo. Unaweza:

  • Kuchagua kama nyenzo hiyo ionekane kwa wanafunzi wako tu (bure, kama ilivyo desturi) au kwenye profile yako ya umma ili mtu yeyote aone na kununua.

  • Kuweka bei ya nyenzo hiyo ikiwa unataka kuiuza kwenye profile yako.

  • Kuongeza thumbnail (picha ndogo) itakayovutia wanunuzi.

Mtu akinunua, malipo yanaingia moja kwa moja kwenye Earnings yako (baada ya kamisheni ndogo ya jukwaa), na anaweza ku-download nyenzo hiyo mara tu baada ya kulipia.

10. Fuatilia Mapato Yako

Kwenye "Earnings", unaweza kuona kiasi ulichopata kutoka kwenye masomo na mauzo ya nyenzo zako, pamoja na historia ya malipo yaliyofanyika. Unaweza kuomba kutoa fedha (payout) wakati wowote kulingana na masharti ya jukwaa.

11. Jenga Sifa Yako kwa Maoni Mazuri

Baada ya kila somo, familia inaweza kuacha maoni (review) na rating. Maoni mazuri yanaongeza uaminifu wako na kukufanya uonekane zaidi kwa wateja wapya. Hivyo daima toa huduma bora, wasiliana kwa heshima, na fundisha kwa moyo.

Kwa Kifupi

  1. Jisajili na kamilisha maelezo ya msingi.

  2. Chagua kundi sahihi la ufundishaji (Academic au Skills).

  3. Weka bei ya kweli.

  4. Kamilisha Verification ili upate tick.

  5. Weka ratiba yako na uwe tayari kujibu maombi haraka.

  6. Fundisha kwa wakati na weledi.

  7. Tumia Resources kuuza nyenzo zako.

  8. Fuatilia mapato yako na uombe payout unapohitaji.

Karibu Ticha Smart — hii ni fursa yako ya kuonekana, kuaminika, na kukua kama mwalimu Tanzania nzima. Ni zamu yako sasa kuangaza! 🎓

Share:fxin

Ready to find the right teacher?

Browse verified teachers across Tanzania and book your first session today.

Find a Teacher